Scholz azungumzia vita vya Ukraine na mgogoro wa tabia nchi
16 Machi 2023Matangazo
Akiwahutubia wabunge mjini Berlin, Kansela Scholz amesema imani haiwezi kuletwa kwa njia ya sheria bali inapaswa kuwa matokeo ya mafanikio yaliyokwishaletwa.
Amesema Ujerumani na Ulaya zina msingi wa kuwa na imani. Amesisitiza kwamba sasa ni juu ya watu wa Ulaya kusimama pamoja katika kuzikabili chagamoto ili kuweza kuleta enzi mpya nzuri.
Kansela huyo wa Ujerumani amekumbusha kwamba nchi yake imeweza kuondokana na kutegemea mahitaji ya nishati kutoka Urusi mnamo kipindi cha miezi minane tu na kwamba sasa inao wagavi wengine wa nishati hiyo.