Scholz, Biden waapa kuendelea kuisaidia Ukraine
4 Machi 2023Matangazo
Matamshi hayo waliyatoa siku ya Ijumaa (Machi 3) wakati Scholz alipokutana na Biden katika Ikulu ya Marekani, White House.
Viongozi hao walizungumzia umoja wao na kuelezea dhamira yao ya kuiunga mkono Ukraine, kutokana na mvutano wa hivi karibuni kuhusu kuipatia Ukraine vifaru.
Soma zaidi: Kansela Scholz awasili Marekani
Scholz alisema "ushirikiano na Marekani uko katika hatua nzuri" na jambo muhimu ni kuwa wamechukua hatua pamoja.
Biden alimshukuru Scholz kwa uongozi wake imara na thabiti ambao umeleta mabadiliko makubwa.
Biden pia alimpongeza Scholz kwa uamuzi wake wa kuongeza matumizi ya jeshi la Ujerumani na kubadilisha vyanzo vya nishati na kupunguza kuitegemea gesi ya Urusi.