1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz kwenda Moldova na kujadili athari za vita vya Ukraine

21 Agosti 2024

Kansela wa Ujerumano Olaf Scholz leo anasafiri na kuelekea Moldova, jamhuri iliyokuwa katika umoja wa Sovieti. Nchi hiyo inayopakana na Ukraine, ina hofu kufuatia kuvamiwa kwa jirani yake na Urusi.

Olaf Scholz akizungumza kwa simu
Kansela Olaf Scholz (SPD) wakati aliiüpokuwa akipiga simu katika mkutano wa kilele wa mataifa ya G7.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Scholz atafanya mazungumzo na Rais wa Moldova Maia Sandu na Waziri Mkuu Dorin Recean katika mji mkuu wa nchi hiyo. Mazungumzo yake yatajikita katika athari za vita vya Urusi nchini Ukraine kwa nchi hiyo ndogo na wakaazi wake milioni 2.6. Serikali ya Moldova ambayo inatafuta kuwa mwanachama wa Umojawa Ulaya inaituhumu Urusi kwa kutoa taarifa za uongo kwa kukusudia na kuiyumbisha nchi hiyo. Urusi ina kituo cha majeshi yake katika eneo lililojitenga la Transnistria tangu miaka ya tisini. Scholz aliizuru Moldova mwaka jana kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Ulaya ila ziara yake ya sasa ndiyo ya kwanza ya baina ya nchi na nchi kufanywa na Kansela wa Ujerumani katika kipindi cha miaka 12.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW