Scholz kukutana na wakuu wa majimbo 16 kujadili wahamiaji
6 Novemba 2023Kansela Olaf Scholz leo atakutana na viongozi wa majimbo yote 16 ya Ujerumani kutafuta njia za kukabiliana idadi kubwa ya wahamiaji,suala ambalo limekuwa tatizo kubwa la kisiasa kwa serikali yake.
Katika mkutano huo Kansela anakabiliwa na shinikizo kubwa la kutoa majibu kuhusu suala hilo.
Mawaziri wakuu wa serikali za majimbo wanaitaka serikali kuu mjini Berlin iongeze bajeti kwa serikali zao kushughulikia gharama za kuwapokea wahamiaji.
Soma pia:Uhamiaji Umoja wa Ulaya bado suala tete
Makaazi ya kuwaweka wahamiaji na wakimbizi yamefurika nchini Ujeremani na Kansela Scholz anayekabiliwa na shinikizo kubwa kutoka upande wa upinzani na kwengineko akitakiwa kusitisha mpango wa kuwapokea wakimbizi,amesema wahamiaji wengi zaidi wataingia Ujerumani.
Wakimbizi zaidi ya milioni mojakutoka Ukraine waliingia Ujerumani tangu Urusi ilipoanzisha vita nchini humo.