Scholz kukutana na Xi pembezoni mwa mkutano wa G20
15 Novemba 2024Matangazo
Mazungumzo hayo yatafanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa mataifa yanaoyoongoza kiuchumi duniani G20 utakaofanyika nchini Brazil.
Scholz na Xi watakutana siku ya Jumanne na kujadili vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati, uhusiano kati ya China na Ujerumani pamoja na usawa wa kibiashara duniani.
Scholz ambaye alikutana na Xi mara ya mwisho mwezi Aprili mjini Beijing, hakudiriki kutoa maneno makali kwa China kama ilivyofanya Marekani na mataifa mengine ya Ulaya, na badala yake ameonesha nia ya kuwa mshirika muhimu wa Beijing.
Mwaka jana, China ilikuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Ujerumani, taifa lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya, ambalo hata hivyo uchumi wake unatarajiwa kushuka kwa mwaka wa pili mfululizo.