Bunge la Marekani laombwa kuidhinisha msaada kwa Ukraine
10 Februari 2024Matangazo
Viongozi hao wawili, wameonya kuwa taifa hilo haliwezi kuendelea kukabiliana na uvamizi wa Urusi bila msaada huo.
Kansela Scholz ambaye nchi yake ni muungaji mkono mkubwa wa kijeshi wa Ukraine, ikifuatiwa na Marekani amesema anatumai kutafikiwa makubaliano ya kuidhinisha msaada huo wa mabilioni ya dola.
Awali, Scholz aliwaambia waandishi habari kwamba ametiwa moyo na hatua ya Baraza la Seneti la Marekani kuanza kuuangazia mpango utakaoidhinisha msaada wa dola bilioni 60 kwa Kiev.
Biden, Scholz kujadiliana msaada kwa Ukraine
Hata hivyo, bado kuna mashaka ikiwa wabunge wa Republican wanaodhibiti Baraza la Wawakilishi wataupitisha muswada huo.