1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz na Merz wapambana kwa maneno bungeni

11 Februari 2025

Wanasiasa wawili vigogo wanaowania kiti cha Ukansela wa Ujerumani wameshambuliana kwa maneno leo wakati wa kikao cha mwisho cha bunge mjini Berlin siku chache kabla ya uchaguzi utakaofanyika Februari 23.

Letzte Plenarsitzung - Heftiger Schlagabtausch im Bundestag
Friedrich Merz, mgombea wa Chansela akizungumza na Kansela Olaf Scholz pamoja na Robert Habeck.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kwenye kikao hicho, Kansela anayewania kuchaguliwa Olaf Scholz wa chama cha SPD amemshambulia kwa maneno mgombea mwenzake wa chama cha kihafidhina cha CDU, Friedrich Merz, akisema mapendekezo yake ya kisera ni "hatari kwa ushirikiano wa kanda ya Ulaya." Amesema sera za CDUzinazoshinikiza Ujerumani ichukue msimamo binafsi kuhusu suala la uhamiaji zinakwenda kinyume na sheria za Ulaya na zitavuruga mshikamano wa kanda hiyo. Kwa upande wake Merz, amekosoa mapendekezo ya Scholz ya kutaka kuongeza kodi kwa matajiri akimtuhumu "kupalalilia wivu na chuki" dhidi ya watu walio na kipato kikubwa. Amezilaumu pia sera za kiuchumi za kiongozi huyo anazosema ndiyo sababu ya kuongezeka idadi ya watu wasio na ajira nchini Ujerumani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW