1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMisri

Scholz na Rais wa Misri wazungumzia hali ya mgogoro wa Gaza

29 Januari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Misri Abdel-Fattah al Sisi wamefanya mazungumzo leo Jumatatu kwa njia ya simu kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akizungumza kwa njia ya simu
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akizungumza kwa njia ya simuPicha: Hannibal Hanschke/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Seibert, viongozi wote wawili wamekubaliana kwamba ufikishaji wa msaada wa kiutu na mahitaji mengine katika Ukanda wa Gaza unapaswa kuimarishwa.

Kadhalika wamesema raia walioko kwenye eneo hilo la vita kati ya kundi la wanamgambo la Hamas na Israel wanapaswa kulindwa.

Lakini pia katika taarifa iliyotolewa, Kansela Olaf Scholz amesisitiza kwamba Ujerumani inaunga mkono suluhisho la kuweko madola mawili kuupatia ufumbuzi mgogoro huu.

Scholz na Al Sisi imeelezwa kwamba kwa pamoja wamekubaliana kwamba juhudi zinatakiwa kufanyika kuzuia kutanuka kwa vita hivyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW