Silaha za Ujerumani zisitumike kufanya mashambulizi Urusi
27 Mei 2023Matangazo
Scholz ameyasema hayo siku ya Ijumaa akiwa ziarani katika mji mkuu wa Estonia Tallin na kuongeza kwamba silaha wanazozitoa ni kwa ajili ya Ukraine kujilinda pekee.
Mwanzoni mwa mwaka, Scholz alisema kulikuwa na "makubaliano" na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwamba,silaha za Ujerumani hazitatumika kwa mashambulio kwenye eneo la Urusi.
Soma zaidi: Scholz atangaza nchi yake itapeleka silaha zaidi UkraineKauli ya Kansela Scholz mara kadhaa imerudiwa na Marekani ikiwemo mnamo siku ya Alhamisi ambapo msemaji wa Ikulu ya White House John Kirby alisema vifaa vilivyotengenezwa na Marekani, vinavyotolewa na Marekani havitakiwi kutumika katika kuishambulia Urusi.