1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz, Zelenskiy kulihutubia kongamano la uchumi la Davos

18 Januari 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy watalihutubia leo Kongamano juu ya Uchumi wa Dunia mjini Davos-Uswisi.

MSC 2022 - Olaf Scholz und Wolodymyr Selenskyj
Picha: Sven Hoppe/REUTERS

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy watalihutubia leo Kongamano juu ya Uchumi wa Dunia mjini Davos-Uswisi, hotuba zao zikiwa miongoni mwa zilizo muhimu zaidi katika kongamano la mwaka huu.

Ujerumani inakabiliwa na shinikizo ikitakiwa kuipatia Ukraine vifaru vya kivita, huku Ukraine ikijiandaa kuingia mwaka wa pili wa vita tangu ilipovamiwa na Urusi.

Hadi sasa Ukraine imepokea tu vifaru vilivyoundwa katika iliyokuwa Umoja wa Kisovieti, ambavyo vilikuwa katika maghala ya nchi za Ulaya Mashariki ambazo sasa ni wanachama wa umoja wa kujihami wa NATO. Licha ya miito kutoka Ukraine na washirika wa NATO, Ujerumani imekataa kuipa Ukraine vifaru vya kisasa chapa Leopard-2.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW