Schröder apinga kuhukumiwa kifo Saddam Hussein.
20 Desemba 2003Matangazo
BERLIN: Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amesema anapinga dhana ya kuhukumiwa kifo mtawala wa zamani wa Iraq Saddam Hussein. Huo ni msimamo wake wa kimsingi kwa kila mtu, hata ikiwa inamhusu Dikteta aliyewatesa kikatili wapinzani wake, Kansela Schröder aliliambia gazeti la Kijerumani BILD AM SONNTAG. Bila ya kuitaja kwa jina hukumu ya kifo, Rais George W. Bush wa Marekani alitoa mwito kuwa ahukumiwe adhabu kali kabisa Saddam Hussein baada ya kutiwa kwake mbaroni kama wiki moja iliyopita nchini Iraq. Baraza Tawala la Mpito la Iraq lingependelea kuona Saddam Hussein akihukumiwa nchini. Kwa hivi sasa hukumu ya kifo imefutwa nchini Iraq.