1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schulz : Mazungumzo ya biashara ya CETA bado yanaendelea

22 Oktoba 2016

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Martin Schulz ana matumaini Umoja wa Ulaya na Canada zitasaini makubaliano ya biashara (CETA) ambayo mazungumzo yake yalivunjika baada ya kupingwa na mkoa wa Wallonia wa Ubelgiji.

Chrystia Freeland  und  Martin Schulz
Picha: picture alliance/dpa/B.Bourgeois

Schulz amesema Jumamosi ( 22.10.2016) baada ya kukutana na Waziri wa Biashara wa Canada Chrystia Freeland kwamba anataraji Umoja wa Ulaya utaondokana na upinzani wa mkoa wa Ubelgiji wa Wallonia ambao unakwamisha kusainiwa kwa mabaliano hayo ya CETA kati ya Umoja wa Ulaya na Canada.Amesema mazungumzo hayo yanapaswa kusainiwa wiki ijayo.

Schulz ambaye hahusiki moja kwa moja katika mazungumzo ya CETA lakini ana ushirikiano mzuri wa kikazi na Freeland amekuwa na mkutano wa dharura na waziri mkuu wa Wallonia Paul Magnette katika juhudi za kuyauhisha makubaliano hayo.

Kabla ya mkutano huo amesema " Mlango kwa kila hatua ya kusonga mbele uko wazi lakini ni jambo lililo wazi kabisa kwamba matatizo yalioko mezani ni matatizo ya watu wa Ulaya na bado kazi inatakiwa ifanyike kwa upande wetu ...lakini nina matumaini makubwa sana tutayatatuwa matatizo haya ndani ya Umoja wa Ulaya."

 

Mpira uko uko uwanja wa Ulaya

Rais wa Umoja wa Ulaya Martin Schulz na Waziri Mkuu wa jimbo la Wallonia la Ubelgiji Paul Magnette.Picha: Getty Images/AFP/N.Maeterlinck

Waziri wa biashara wa Canada ambaye ameahirisha mipango yake ya kurudi nyumbani Canada Jumamosi ameseama ni wajibu wa Umoja wa Ulaya kuyanusuru makubaliano hayo ya biashara huru ambayo yanakwamishwa na mkoa wa Ubelgiji wa Wallonia wenye  kuzungumza Kifaransa.Amesema Canada iko tayari kusaini mazungumzo hayo na kwamba mazungumzo juu ya nukta muhimu yamekamilika.Amesema "Tumetimiza wajibu wetu. Tumekamilisha kuzungumzia makubaliano mazuri.Sasa mpira uko katika uwanja wa Ulaya.

Nchi zote 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya zinaunga mkono Mukubaliano hayo Kabambe ya Kiuchumi na Makubaliano ya Biashara (CETA) lakini Ubelgiji haikuweza kuridhia bila ya kuungwa mkono na serikali za mikoa yake mitano ambapo ule wa Wallonia umepinga moja kwa moja.

Wallonia inaendelea kuwa na wasi wasi juu ya kitisho cha kuongezeka kwa nyama ya nguruwe na n'gombe inayoagiziwa na Ubeligiji kutoka Canada na kuanzishwa kwa mfumo wa mahakama kusuluhisha mizozo kati ya nchi na wawekezaji wa kigeni ambapo wakosoaji wamesema huenda ikatumika na makampuni ya kimataifa kulazimisha sera za serikali.

 

Freeland hapo Ijumaa alitoka katika mazungumzo hayo yaliohudhriwa na waziri mkuu wa Wallonia Magnette na wajumbe wa Umoja wa Ulaya na kutangaza kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya ni jambo lisilowezekana.

 

Siasa za Ubelgiji zakwamisha mazungumzo

Rais wa Baraza la Ulaya Martin Shulz na Waziri wa Biashara wa Ujerumani Sigmar Gabriel.Picha: picture-alliance/dpa/J. Stratenschulte

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Sigmar Gabriel amesema yeye pia ana mazumaini juu ya mazungumzo hayo kufikia makubaliano. Wizara yake imesema Gabriel ametimiza dhima kubwa katika kumshawishi Freeland kutorudi Canada masaa machache baada ya nchi hiyo kutangaza kwamba mazungumzo hayo yamekufa.

Gabriel ameongeza kusema kwamba siasa za Ubelgiji zisiachiliwe kuyashikilia mateka makubaliano yote hayo ya kibiashara.Kwa mujibu wa wizara yake "Hili ni tatizo la kisiasa la ndani ya nchi ya Ubelgiji na sio tatizo kwa Canada. Makubaliano ya CETA ni makubaliano safi kabisa na hayawezi kusambaratishwa kwa sababu ya ukosefu wa ufanisi wa Ulaya katika kutafuta njia za kulaumu maslahi kati ya maeneo."

Makubaliano ya CETA yalitakiwa yasainiwe katika mkutano wa kilele Umoja wa Umoja wa Ulaya na Canada wiki ijayo mbele ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Makubaliano hayo ya CETA yamesarifiwa kurahisisha mtiririko wa bidhaa kati ya Canada na nchi wanachama 28 wa Umoja wa Ulaya. Yanatarajiwa kuongeza biashara kwa asilimia 20.

Mwandishi : Mohamed Dahman / dpa/ Reuters

Mhariri : Sudi Mnette