1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal kufanya uchaguzi wa bunge Jumapili

14 Novemba 2024

Senegal itapiga kura ya bunge Jumapili (17.11.2024) itakayoamua iwapo rais mpya na serikali yake wanaweza kuchukua udhibiti wa bunge na kusukuma ajenda zao za mageuzi.

Senegal | Bassirou Diomaye Faye
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

.Umuhimu wa uchaguzi huo unatishia kuzusha vurugu upya kufuatia kipindi cha utulivu

Kampeni zimepamba moto katika siku za hivi karibuni na haya yanakuja wakati mbaya kwa serikali mpya ya nchi hiyo, ambayo inakabiliana na mdororo wa kiuchumi ambao unatishia kuhujumu uwezo wake wa kutimiza ahadi zake za kuustawisha uchumi na kubuni ajira.

Senegal kuchagua wabunge wapya Jumapili

Waziri Mkuu Ousmane Sonko kwa matamshi yake makali, wiki hii alisema kwamba wafuasi wake walishambuliwa na akawataka walipize kisasi. Ametahadharisha pia kwamba kujizuia kufanya vurugu hakustahili kuchukuliwa kama udhaifu. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW