1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korti yaamuru Sonko kurejeshwa kwenye daftari la kura

14 Desemba 2023

Mahakama ya Senegal imeamuru kurejeshwa katika daftari la uchaguzi, jina la kiongozi wa upinzani wa nchi hiyo aliyefungwa jela, uamuzi ambao unaweza kumfungulia njia kugombea katika uchaguzi wa urais wa Februari.

Senegal I Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani wa Senegal Ousmane SonkoPicha: Seyllou/AFP

Tangazo hilo limetolewa na wakili wake Sonko Cire Cledor Ly.

Hata hivyo wakili mmoja wa serikali amesema kuwa serikali itakaa rufaa dhidi ya uamuzi huo

Ousmane Sonko amekabiliwa na msururu wa kesi mahakamani katika muda wa miaka miwili iliyopita kwa mashtaka yanayojumuisha kashfa na ubakaji, ambayo anakanusha.

Kiongozi huyo alikamatwa mnamo mwezi Julai kwa uasi na jina lake kuondolewa katika orodha ya wapiga kura, hatua inayomzuia kushiriki katika uchaguzi huo wa Februari.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW