1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal: Sonko alazwa chumba cha wagonjwa mahututi

18 Agosti 2023

Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, anaripotiwa kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya mgomo wake wa kula.

Sonko anatazamwa kama kitisho kwa serikali ya Senegal kisiasa.
Sonko anatazamwa kama kitisho kwa serikali ya Senegal kisiasa.Picha: Cooper Inveen/REUTERS

Hayo yanaripotiwa wakati taifa hilo bado likiwa katika joto la kisiasa la kabla ya uchaguzi mkuu.

Moja kati ya wanasheria wake Cire Cledor Ly amesema Sonko aliyepoteza fahamu yupo katika uangalizi mkubwa wa kitabibu katika hospitali kuu ya Dakar.

Shirika la Habari la Ufaransa la AFP, limefanya jitihada kadhaa za kupata taarifa za kina kutoka kwa upande wa serikali lakini liligonga mwamba.

Sonko ambaye anatazamwa kama kitisho kwa serikali ya Senegal kisiasa alianza mgomo huo Julai 30 baada ya kushutumiwa kwa kuchochea ghasia mbaya kati ya wafuasi wake na vikosi vya usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW