1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal wachaguwa wabunge wapya

17 Novemba 2024

Raia nchini Senegal wanapiga kura hii leo Jumapili kwenye uchaguzi wa bunge, ambapo serikali inasaka wingi wa kutosha bungeni kuiwezesha kutekeleza mageuzi iliyoyaahidi kwenye uchaguzi wa mwezi Machi.

Uchaguzi Senegal
Raia wa Senegal akipiga kura kwenye uchaguzi wa bunge wa tarehe 17 Novemba 2024.Picha: John Wessels/AFP

Wapigakura zaidi ya milioni saba wanawachagua wabunge 165 watakaohudumu kwa kipindi cha miaka mitano.

Uchaguzi huu unaofanyika miezi minane baada ya Rais Bassirou Diomaye Faye na kundi lake la waliokuwa wapinzani wakubwa wa serikali kuingia madarakani, ni muhimu kwa kiongozi huyo kijana anayeelemea mrengo wa kushoto na ambaye alitumia kampeni yake kuahidi mageuzi makubwa ya kiuchumi, mfumo wa haki za kijamii na mapambano dhidi ya ufisadi.

Soma zaidi: Senegal wachaguwa wabunge wapya

Hata hivyo, bunge linaloongozwa na upinzani limeifanya miezi ya mwanzo ya serikali hiyo mpya madarakani kuwa migumu, jambo ambalo lilimfanya Faye kulivunja bunge mwezi Septemba na kuitisha uchaguzi wa mapema mara tu katiba ilipomruhusu kufanya hivyo.