1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Senegal yaweka ajenda kabambe ya maendeleo

15 Oktoba 2024

Serikali nchini Senegal, imezindua mpango mkubwa wa kujitegema kimaendeleo, huku ikiahidi kuongeza mapato ya wastan ya watu binafsi kwa takriban asilimia 50 katika kipindi cha miaka mitano.

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye FayePicha: Sylvain Cherkaoui/AP Photo/picture alliance

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, ameutaja mfumo huo mpya wa sera ya umma kama "maono kwa Senegal ambayo inatamani sio tu kushiriki katika ulimwengu wa kesho, lakini kuchukua jukumu kubwa ndani yake".

Faye ameongeza kuwa agenda ya mabadiliko ya kitaifa ya Senegal 2050, itafanya kazi kuifanya nchi hiyo kuwa mshirika mkuu wa kikanda na mfano wa maendeleo kwa Afrika.

Sonko asema mpango mpya wa serikali utaiondoa Senegal katika utegemezi wa mataifa ya nje

Waziri mkuu wa Senegal Ousmane Sonko, amesema mkakati huo ulilenga kuvunja kile alichokiita "mtindo wa kujirudia wa utegemezi na maendeleo duni.

Mpango huo wa miaka 25 unalenga kuliondoa taifa hilo la Afrika Magharibi kutoka katika utegemezi wa mataifa ya kigeni na madeni na kutumia raslimali za ndani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW