1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seneta Vance: Trump hatoitelekeza NATO dhidi ya adui

18 Februari 2024

Mtetezi mkubwa wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika bunge la Marekani, ametoa hakikisho kwa washirika wa NATO kuwa Marekani itashiriki katika utetezi wa mataifa wanachama endapo Trump akirejea.

maandamano ya kumuunga mkono mgombea Seneti Ohio
Umati wa watu ukiinua bendera wakati mgombea wa Republican wa Marekani Seneta JD Vance akizungumza kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dayton Novemba 7,Picha: Drew Angerer/AFP/Getty Images

Mtetezi mkubwa wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika bunge la Marekani, ametoa hakikisho kwa washirika wa NATO kuwa Marekani itashiriki katika utetezi wa mataifa wanachama pale itakapotokea uvamizi hata kama rais huyo atarejea kwa awamu ya pili katika kiti cha urais mwezi Novemba. Akizungumza na waandishi wa habari kandoni mwa mkutano wa usalama wa huko Munich Ujerumani, Seneta JD Vance, amesema, ujumbe kutoka kwa Trump na wanachama wenzake wa Republican ni kuwa, Ulaya inafaa iongeze nguvu binafsi, zaidi pale linapokuja suala la kujilinda. Vanceameongeza kusema iwapo Ulaya inaamini rais wa Urusi Vladimir Putin ni "tishio" basi mataifa yenye nguvu ya kiuchumi kama Ujerumani lazima yaingilie kati. Mkutano wa usalama unaofanyika Munich unahitimishwa hii leo, ambapo Marekani imetowa wawakilishi wake wakiwemo zaidi ya wajumbe 30 wa bunge la Marekani katika mkutano huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW