1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seneti ya Kenya kupiga kura kumuondoa naibu rais mamlakani

17 Oktoba 2024

Baraza la Seneti nchini Kenya limeanzisha kikao cha siku ya pili leo kuelekea kura ya kumuondoa madarakani naibu wa rais wa nchi hiyo Rigathi Gachagua.

Kenya | Rigathi Gachagua alipokuwa katika bunge la taifa kujitetea
Wawakilishi katika bunge la taifa nchini Kenya walishapiga kura ya kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua madarakani na sasa hatma yake iko mikononi mwa masenetaPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Gachagua anakabiliwa na madai ya ubadhirifu wa fedha za umma, kuchochea ukabila na kuihujumu serikali, madai ambayo anayakana. Iwapo theluthi mbili ya maseneta wataunga mkono kuondolewa ofisini kwa Gachagua katika kura ya jioni ya Alhamisi, Gachagua atakuwa naibu wa rais wa kwanza nchini Kenya kuondolewa madarakani kwa njia hiyo iliyoanzishwa kupitia katiba mpya ya nchi hiyo ya mwaka 2010.

Siku ya leo itajumuisha ushahidi utakaotolewa na Gachagua mwenyewe ambaye atajibu madai kadhaa yaliyowasilishwa na mbunge Mwengi Mutuse.

Mahakama za Kenya zimekataa kusimamisha vikao hivyo vya Baraza la Seneti kama alivyotaka Gachagua, ila zimesema kwamba huenda zikauangazia upya mchakato huo iwapo umefuata sheria mara utakapokamilika. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW