Sengbe Pieh, mkulima na mfanyabiashara kutoka Sierra Leone alikamtwa na kutumbukizwa kwenye utumwa 1839. Wakati akisafirishwa na wenzake kwenye meli ya Amistad kuelekea Cuba, Pieh aliongoza uasi dhidi ya waliowakamata, tukio ambalo lilizua harakati za kukomesha biashara ya utumwa.