1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL: Korea Kusini kuiuzia Korea Kaskazini nguvu za umeme.

17 Machi 2005

Korea Kusini imeanza mpango wake wa kuiuzia nguvu za umeme nchi jirani ya Korea Kaskazini pamoja na kuwepo na mzozo wa silaha za kinuklia.

Kwa mujibu wa kampuni ya umeme ya Korea Kusini wati 15,000 za umeme kwa saa zitauziwa kiwanda kilicho katika mpaka wa nchi hizi mbili na ambacho kinaendeshwa kwa ushirikiano wa Korea Kusini na Korea Kaskazini.

Hii ni mara ya kwanza kwa Korea Kusini kuiuzia nguvu za umeme nchi jirani yake ya kikomunisti tangu Korea ilipogawanywa miaka 57 iliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW