SEOUL: Korea Kusini yakataa mazungumzo na Korea Kazkazini
7 Julai 2006Matangazo
Korea Kusini imekataa pendekezo la Korea Kazkazini la kufanya mazunguzo ya pamoja ya kijeshi yenye lengo la kupunguza hali ya wasiwasi katika eneo la mpakani.
Serikali ya mjini Seoul imesema wakati wa mazunguzo hayo haufai. Pendekezo la serikali ya Pyongyang limetolewa siku mbili baada ya Korea Kazkzini kufanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu yaliyokosolewa na jamii ya kimataifa.