1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul. Marekani yaeleza matumaini yake katika mkutano wa mataifa sita kujadili suala la mpango wa kinuklia wa Korea ya kaskazini.

13 Julai 2005

Marekani na Korea ya kusini zimesema kuwa zinamatumaini juu ya mazungumzo ya nchi sita kuhusu mipango ya Korea ya kaskazini ya silaha za kinuklia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bibi Condoleezza Rice amewaambia waandishi wa habari mjini Seoul kuwa anaamini juhudi za kuimarisha hali ya usalama katika eneo la Korea zinaweza kuzaa matunda.

Lakini ameongeza kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Waziri mwenzake wa Korea ya kusini Ban Ki-Moon amesema kuwa Rice amesifu mapendekezo ya hivi karibuni ya Korea ya kusini ya kuipatia Korea ya kaskazini umeme pamoja na msaada wa chakula , kuwa ni ya manufaa.

Korea ya kaskazini imetangaza mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa itajiunga tena na mazungumzo hayo ya nchi sita, baada ya kukataa kufanya hivyo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW