SEOUL: Mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani
21 Agosti 2006Matangazo
Korea ya Kusini na Marekani zimeanzisha mazoezi ya kijeshi ya pamoja.Kama wanajeshi 8,000 wa Marekani na wanajeshi wa Korea ya Kusini ambao idadi yao haikutajwa,wanashiriki katika mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka.Hayo ni kwa mujibu wa duru za kijeshi za nchi hizo mbili.Wiki iliyopita shirika rasmi la habari nchini Korea ya Kaskazini –KCNA kwa mara nyingine tena lililalamika kuhusu mazoezi hayo ya pamoja na kusema kuwa ni “uchokozi mkubwa wa kijeshi.”Korea ya Kaskazini tarehe 5 Julai,ilijaribu makombora 7 ya masafa marefu katika bahari ya Japan.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja lililaani hatua hiyo na kuweka vikwazo dhidi ya Pyongyang.