1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul: Rumsfeld aikashifu Korea ya Kaskazini

18 Novemba 2003

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Donald Rumsfeld, amesema leo kuwa Korea ya Kaskazini ni nchi ovu kwa sababu inatumia fedha nyingi kununua silaha na huku watu wake wanakufa kwa njaa. Amesema kuwa Wanajeshi wa Kimarekani walioko Korea ya Kusini wanaishi katika mpaka wa uhuru na utumwa. Bw. Rumsfeld amesema hayo alipokuwa anawahutubia Wanajeshi wa Kimarekani, Waume kwa Wanawake, katika kituo cha Jeshi la Angani cha Osan ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini humo. Bw. Rumsfeld amesema kuwa miaka 50 baada ya kumalizika vita vya Korea vya mwaka 1950-53, ambapo majeshi ya Umoja wa Mataifa yalioongozwa na Marekani dhidi ya Wakorea Kaskazini waliokuwa wanaungwa mkono na Wachina, tofauti ni kubwa sana kati ya Kaskazini ya kikomunisti na kusini ya kibepari. Watu wa kaskazini wanaokandamizwa wanawaangalia Watoto wao wakioza na kula magome ya miti wakati serikali yao ovu inatumia kiasi kikubwa cha fedha kwa kununua silaha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW