1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAsia

Seoul: Urusi iliipa Korea Kaskazini mifumo ya ulinzi wa anga

22 Novemba 2024

Korea Kusini imesema, Urusi iliipa Korea Kaskazini mifumo ya ulinzi wa anga ili ipewe wanajeshi waisaidie katika vita dhidi ya Ukraine. Haya yamesemwa na mshauri wa usalama wa taifa wa Rais Yoon Suk Yeol, Shin Wonsik.

Kim Jong Un und Putin
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Zemlianichenko/AP Photo/picture alliance

Shin, amesema hayo katika kipindi cha televesheni cha kituo cha SBS na kuongeza kuwa Korea Kusini imegundua kuwa Urusi ilipokea si tu makombora bali pia vifaa vingine vya kuimarisha ulinzi wake wa anga katika mji mkuu Korea Kaskazini, Pyongyang.

Shin pia amesema Urusi ilitoa msaada wa kiuchumi kwa Korea Kaskazini pamoja na teknolojia mbali mbali za kijeshi zinazojumuisha zile zinazohitajika kusaidia Pyongyang kutengeneza mfumo wa kutegemewa wa ulinzi wa anga.

Soma zaidi: 

Marekani, KoreaKorea Kaskazini yaidhinisha mkataba wa kihistoria wa ulinzi na Urusi Kusini na Ukraine zinasema Korea Kaskazini ilituma zaidi ya wanajeshi 10,000 kwenda Urusi mnamo mwezi Oktoba, ambao baadhi yao wanadaiwa kuanza kutumika katika mapambano.

Hayo yanajiri wakati Rais Vladimir Putin akisema kuwa vita vya Ukraine vinageuka kuwa mgogoro wa kidunia. Hii ni baada ya Marekani na Uingereza kuiruhusu Ukraine kuishambulia Urusi na silaha inazopewa na nchi hizo. Putin amezionya nchi za Magharibi kuwa Moscow inaweza kujibu mashambulizi hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW