Seoul. Waziri Jung yuko katika ziara barani Asia.
20 Aprili 2007Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amewasili Korea ya kusini ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika bara la Asia.
Maafisa wa serikali ya Ujerumani wamesema kuwa waziri huyo anatembelea nchini humo ili kujadili pendekezo la mauzo ya makombora ya zamani ya Patriot.
Korea ya kusini, ambayo inakabiliwa na kitisho kikubwa kijeshi kutoka kwa Korea ya kaskazini yenye silaha za kinuklia, inataka kubadilisha makombora yake ya kutoka ardhini kwenda angali ambayo yana umri wa miaka 40.
Mpango huo unatarajia kuigharimu nchi hiyo kiasi cha dola bilioni 1.2.
Hapo mapema , Ujerumani na Japan zimekubaliana kuimarisha zaidi ushirikiano wao kijeshi.
Baada ya mazungumzo na mwenzake nchini Japan , Jung amesema pande hizo mbili zitafanyakazi kwa pamoja katika miradi mbali mbali ya ulinzi.