Seoul.Ban Ki Moon kufanya jitihada binafsi kumaliza mgogoro wa Korea ya Kaskazini.
10 Novemba 2006Matangazo
Katibu Mkuu mteule mpya wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema, atatumia ushawishi wake kusaidia kupatikana kwa amani juu ya mzozo wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini.
Maelezo ya Ban Ki Moon yamekuja katika hotuba yake aliyoitoa katika hadhara kuu mjini Seoul wakati akitangaza kuachilia madaraka ya uwaziri wa mambo ya nje wa Korea ya Kusini.
Vile vile amehimiza kutimizwa mazimio ya Umoja wa Mataifa na kuyashughulikia masuala ya kimataifa kama ugaidi na Umasikini.
Ban atachukua madaraka kutoka kwa katibu mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ifikapo tarehe mosi January.