1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL:Hakuna azma ya kuishambulia Korea ya Kaskazini

20 Machi 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice yupo Seoul kwa mazungumzo pamoja na viongozi wa Korea ya Kusini.Ziara yake nchini humo inafanywa wakati ambapo majeshi ya Marekani na Korea ya Kusini yameanza kufanya mazoezi yao ya kila mwaka.Serikali ya Korea ya Kaskazini mjini Pyongyang imesema inayatazama mazoezi hayo kama ni matayarisho ya uvamizi.Hapo kabla Rice katika hotuba yake mjini Tokyo,Ujapani alisema Washington haina azma ya kuishambulia Korea ya Kaskazini.Lakini akaongezea kuwa Marekani itaendelea kuwa na msimamo mkali kuhusu Pyongyang.Vile vile alitoa muito kwa Korea ya Kaskazini kurejea katika majadiliano yanayohusika na miradi yake ya kinuklia.Mwezi uliopita Pyongyang ilijitoa kutoka mazungumzo hayo yanayofanywa na nchi sita.Imesema kabla ya kufikiria kurejea katika meza ya majadiliano inamtaka kwanza Rice aombe msamaha kwa sababu ya kuitaja Korea ya Kaskazini kama ni "ngóme ya udhalimu."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW