Serbia yaagiza wanajeshi kuukaribia mpaka na Kosovo
26 Mei 2023Matangazo
Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo, Milos Vucecic, alipokuwa akitangaza hatua moja kwa moja kupitia televisheni, amesema ni wazi kwamba jamii ya Waserbia walioko Kosovo wanafanyiwa vitendo vya ugaidi.
Polisi walipambana na waandamanaji katika mji wa Zvecan ulioko Kosovo baada ya kukusanyika mbele ya jengo la manispaa, wakijaribu kumzuia meya mpya wa asili ya Albania kuingia ofisini.
Waserbia karibu 50,000 wanaoishi katika manispaa nne kaskazini mwa Kosovo walisusia uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na kile walichosema kuwa madai yao ya uhuru zaidi hayajatekelezwa, hiki kikiwa ni kizingiti kipya kwenye makubaliano ya amani ya Machi kati ya Kosovo na Serbia.