Serbia yainyamazisha Ujerumani
18 Juni 2010Matangazo
Ujerumani ambayo ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kutwaa kombe la dunia, leo imefungwa bao 1-0 na Serbia katika mechi ambayo ilishuhudia Ujerumani ikicheza na wachezaji kumi kwa muda mrefu wa mchezo.
Ujerumani ambayo katika mechi ya kwanza iliifunga Australia mabao 4-0, ilishuhudia mchambuliajai wake Miroslva Klose akipewa kadi nyekundu, na pia Lukas Podoski akikosa penalti.
Mechi nyingine hii leo ni kati Marekani na Slovenia kabla ya Uingereza kucheza na Algeria.
Mwandishi:Aboubakary Liongo