1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serbia yawaachia maafisa wa polisi wa Kosovo

Sylvia Mwehozi
27 Juni 2023

Serbia imewaachia huru maafisa watatu wa polisi wa Kosovo waliokuwa wakizuiliwa na vikosi vya usalama vya Serbia mapema mwezi huu, na hivyo kupunguza mvutano wa hivi karibuni kati ya mataifa hayo mawili ya Balkan.

Kosovo Serbische Festnahme von drei Kosovo-Polizisten löst neuen Streit aus
Picha: Valdrin Xhemaj/REUTERS

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya wiki kadhaa za mvutano mkubwa kati ya pande hizo mbili, ambapo ghasia zilizotokea kaskazini mwa Kosovo zilipelekea zaidi ya wanajeshi 30 wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wakijeruhiwa mwishoni mwa mwezi Mei. 

Mahakama ya Juu ya Serbia ilithibitisha mashitaka dhidi ya maafisa hao watatu wa polisi lakini ikatoa amri ya kuachiliwa.

Soma zaidi: Kosovo yaruhusu magari ya Serbia na bidhaa kuvuka mpaka tena
Mvutano kati ya Kosovo na Serbia wazidi kufukuta

Kukamatwa kwao kulizua vita vya maneno kati ya serikali ya nchi hizo mbili, huku Kosovo ikidai kuwa walikuwa wametekwa nyara na Serbia ikiwashutumu kwa kuvuka mpaka hadi kuingia katika eneo lake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW