JamiiMarekani
Serikali kutoa msaada baada ya vimbunga huko Mississipi
26 Machi 2023Matangazo
Biden amesema msaada wa serikali ya shirikisho utapelekwa katika maeneo yaliyoathirika. Hali mbaya zaidi ya hewa ikiambatana na mvua kubwa na upepo mkali inatarajiwa tena hii leo huko Mississippi.
Shirika la usimamizi wa dharura la serikali limeonya kwamba huenda kukashuhudiwa pia vimbunga. Vikosi vya uokoaji bado vinaendelea kuwasaka manusura.
Soma pia: Vimbunga vyasababisha vifo vya watu 26 huko Mississippi, Marekani
Baadhi ya vitongoji vimeathirika pakubwa ikiwemo kile cha Rolling Fork chenye wakazi takriban 2000, ambako majengo yote yameharibika. Vimbunga huripotiwa mara kwa mara nchini Marekani hasa katika maeneo ya kati na kusini mwa nchi hiyo.