1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali kutojiuzulu Romania licha ya maandamano makubwa

Mohamed Dahman
6 Februari 2017

Kiongozi wa chama Romania cha muungano wa mrengo wa kati na kushoto amesema serikali haitojiuzulu kufuatia maandamano makubwa kabisa kushuhudiwa dhidi ya hatua ambayo ingeliregeza vita dhidi ya rushwa

Rumänien Sorin Grindeanu und Liviu Dragnea in Bukarest
Picha: Reuters/Inquam Photos/O. Ganea

Wizara ya sheria nchini Romania imefutilia mbali mpango wa muswada wa kubadili sheria ya jinai hayo yamebainishwa na kituo cha televisheni cha Digi24 Jumatatu baada ya siku kadhaa za maandamano makubwa dhidi ya amri kuhusu rushwa kulazimisha serikali kuachana na mipango yake ya kuondowa mashtaka ya jinai kwa baadhi ya kesi za rushwa.

Wizara hiyo imesema katika taarifa Jumatatu (06.02.2017)haitaki kuwa na rasimu ya muswada kubadili na kurekebisha sheria nambari 286/2009 kuhusiana na suala la jinai na sheria nambari 135/2010 kuhusiana na taratibu  za sheria ya jinai .

Mwenyekiti wa chama cha Social Demokrat Liviu Dragnea akitoka kwenye mkutano wa asubuhi na washirika wenzake katika utawala amesema wanamiunga mkono bila ya mashaka serikali na waziri mkuu.

Serikali imebadili msimamo

Maandamano makubwa Bucharest.Picha: Reuters/S. Nenov

Hapo Jumapili serikali ilibadili msimamo kufuatia siku sita za maandamano mitaani kuhusiana na amri ya dharura ambayo ingeliondolea makosa ya jinai matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na maafisa wakati wakiwa kazini iwapo kima kinachohusika ni chini ya dola 48,500.Serikali inapanga kuanzisha sheria nyengine bungeni ambapo ina wingi wa viti.

Hata hivyo ikiwa ni dalili ya kuwa na mawazo mengine waziri wa sheria Florin Iorache amesema katika taarifa hakutingwa na shughuli za kuandaa rasimu ya sheria hiyo.Taarifa hiyo iimesema kwa sasa waziri huyo wa sheria analenga maamuzi yaliyochapishwa na Mahakama ya Katiba ambayo yatachambuliwa  hivi karibuni.

Mahakama ya Katiba inategemewa kutowa hukumu ya kuzingatiwa kikatiba kwa pendekezo la kuundowa makosa ya jinai kwa baadhi ya kesi za rushwa baadae wiki hii.

 

Dragnea bado aumezea mate uwaziri mkuu

Maandamano makubwa Bucharest.Picha: picture alliance/dpa/D. Bandic

Dragnea ambaye ana sauti kubwa katika serikali amepigwa marufuku kuwa waziri mkuu kutokana na kupatikana kwake na hatia hapo mwezi wa Aprili mwaka 2016 kwa udanganyifu wa kura.Hata hivyo Dragnea amthibitisha leo hii bado anapigania kuingoza nchi hiyo licha hatia ya jinai inayomzuwiya kuwa waziri mkuu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Romania Dragnea mwenye umri wa miaka 54 hivi sasa anataka kutenguliwa kwa konekana na hatia na kuwa kosa la kitaalamu kwamba mahakama ilishindwa kumtumia hukumu hiyo kwa chapisho ndani ya siku 30 kwa mujibu wa sheria.

Iwapo atafanikiwa hukumu ya kuzuiliwa kwa miaka miwili itafutwa kwenye rekodi na kumfungulia nafasi ya kuwa waziri mkuu.Sheria ya Romania inawapiga marufuku watu  waliopatikana na hatia za jinai kushika nyadhifa za serikali.

Mwandishi : Mohamed Dahman/dpa/AP

Mhariri : Gakuba Daniel

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW