Serikali kuu ya Komoro yashauri Umoja wa Afrika uingilie kijeshi Nzuwani
30 Juni 2007Moroni:
Viongozi wa serikali kuu ya Comoro wameuomba Umoja wa Afrika “uingilie kijeshi kurejesha nidhamu” katika kisiwa cha Nzuwani.Serikali ya Umoja wa Komoro imependekeza mkutano wa baraza la amani na usalama uitishwe pembezoni mwa mkutano mkuu wa 9 wa Umoja wa Afrika mjini Accra,kutathimini upya jukumu la tume ya Umoja wa Afrika iliyokua ikisimamia uchaguzi visiwani humo.Kwa mujibu wa viongozi wa serikali kuu ,”hali inayoendelea kufuatia uasi kisiwani Nzuwani,inatishia umoja wa visiwa vya Komoro.”Taarifa ya serikali kuu iliyolifikia shirika la habari la Ufaransa AFP inakosoa uamuzi wa Umoja wa Afrika wa kuitisha mazungumzo pamoja na viongozi wa Nzuwani nchini Afrika kusini..Uamuzi huo umepitishwa kufuatia ziara ya ujumbe wa Umoja wa Afrika ulioongozwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Afrika kusini June 24 iliyopita kisiwani Nzuwani.