1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Serikali mpya ya Netanyahu kuapishwa Israel

Saleh Mwanamilongo29 Desemba 2022

Ni serikali ya mrengo mkali wa kulia ambayo Israeli imewahi kuwa nayo, ambapo wanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia watajumuishwa kwa mara ya kwanza katika serikali ya mseto.

Malengo ya serikali mpya ya Benjamin Netanyahu kabla ya kula kiapo
Malengo ya serikali mpya ya Benjamin Netanyahu kabla ya kula kiapoPicha: AMIR COHEN/AP/picture alliance

Serikali mpya inataka kutekeleza mabadiliko makubwa ya kisiasa na, pamoja na mambo mengine, kudhoofisha kwa makusudi mfumo wa mahakama nchini Israel. Kulingana na wataalamu, mabadiliko hayo yanaweza pia kusababisha kufutwa kesi ya ufisadi inayoendelea hivi sasa inayomkabili Benjamini Netanyahu.

Hata kabla ya sherehe ya kuapishwa leo Alhamisi, mabadiliko kadhaa ya sheria yenye utata yaliwezeshwa kupitia bunge. Mabadiliko hayo yalizingatiwa kuwa sharti la makubaliano ya pamoja ya muungano huo mpya. Hii ni serikali ya sita iliyoundwa na kiongozi wa kihafidhina wa chama cha Likud, Benjamin Netanyahu. Waziri mkuu huyo wa zamani anarejea madarakani baada ya mwaka mmoja na nusu kwenye upinzani. Katika historia ya Israeli, hakuna aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi ya Nentanyahu,mwenye umri wa miaka 73.

Serikali mpya ina viti 64 kati ya 120 bungeni. Nusu yao ni kutoka chama cha Netanyahu cha Likud, nusu nyingine upande wa mrengo wa kulia wa Muungano wa Kizayuni wa Kidini, pamoja na vyama vingine viwili vyenye msimamo mkali wa kidini. Netanyahu amesisitiza mara kwa mara kwamba yeye mwenyewe ndiye atakayeweka ajenda ya serikali mpya na haitaongozwa na washirika wake wenye msimamo mkali.

Serikali ya mrengo wa kulia

Wanaharakati wa haki za binadaumu wakiandamana mbele ya jengo la Bunge la Israel, maarufu Knesset.Picha: AHMAD GHARABLI/AFP

Wanasiasa kadhaa wenye utata wamepewa nyadhifa za uwaziri. Sheria ilirekebishwa mahsusi kwa kiongozi wa chama cha msimamo mkali wa kidini ''Shas party'', Aryeh Deri, ili aweze kuwa waziri wa

mambo ya ndani licha ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kukwepa kodi. Bezalel Smotrich wa Chama cha Kidini cha mrengo mkali wa kulia cha Kizayuni anatarajiwa kupewa nafasi ya uwaziri katika Wizara ya Ulinzi pamoja na wadhifa wa waziri wa fedha. Smotrich anachukuliwa kuwa mfuasi mwenye bidii wa upanuzi wa makazi kwenye Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.

Miongozo ya serikali iliyochapishwa Jumatano inasema kwamba muungano huo anataka kuendeleza upanuzi wa makazi katika maeneo ambayo Wapalestina wanadai yatakuwa sehemu ya taifa lao la baadaye.

Waziri wa usalama wa taifa atakuwa Itamar Ben-Gvir, mwanasiasa wa mrengo wa kulia ambaye amehukumiwa siku za nyuma kwa kuunga mkono shirika la kigaidi.

Waziri Mkuu anayeondoka,Yair Lapid alisema baada ya mabadiliko ya sheria ambayo serikali mpya ilinaleta, kwamba tayari imethibitishwa kuwa ni serikali fisadi zaidi kuwahi kutokea hata kabla ya kuapishwa kwake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW