1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali mpya ya Israel yapata pigo la kwanza bungeni

6 Julai 2021

Serikali mpya ya Israel imepata pigo bungeni, baada ya kushindwa kurefusha sheria yenye utata inayowazuia Wapalestina walioolewa na Waisraeli kupewa kibali cha ukaazi au uraia wa Israel

Israel Kabinett von MP Naftali Bennett
Picha: Emmanuel Dunand/AFP/AP/picture alliance

Baada ya kura kupigwa bungeni, kila upande ulipata kura 59.

Huo ulikuwa mtihani wa kwanza wa kisiasa kwa Waziri Mkuu Naftali Bennett, takriban mwezi mmoja tangu achukue madaraka kuiongoza  serikali ya muungano inayojumuisha vyama vya mrengo wa shoto, kati na vyama vya kiarabu pamoja na chama chake cha kizalendo.

Israel ilipitisha sheria hiyo mwaka 2003 wakati wa maandamano ya Wapalestina, ikisema Wapalestina walioolewa na Waisraeli walitumia nafasi hiyo ya kisheria kusaidia katika mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Israel.

soma zaidi: Maandamano ya Mayahudi wenye msimamo mkali yazusha wasiwasi Jerusalem Mashariki

Waziri mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu anayeiita serikali ya Bennett kuwa kitisho kwa usalama wa Israel alipiga kura ya kupinga urefushaji wa sheria hiyo.

Baadhi ya wanachama katika muungano unaoongozwa na Bennett akiwemo mwanachama wa chama chake hawakuunga mkono urefushwaji wa sheria hiyo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW