1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali tawala ya Japan yashinda uchaguzi mkuu:

9 Novemba 2003

TOKYO: Kwa kufuatana na tathmini rasmi, katika uchaguzi mkuu wa bunge nchini Japan, serikali ya mwungano ya Waziri Mkuu Junichiro Koizumi imenyakua tena ushindi mkubwa. Kwa kulingana na ripoti za mashirika ya Televisheni ya Japan, mwungano huo umenyakua baina ya viti 243 na 265 kutoka jumla ya viti 480 bungeni. Lakini tathmini hizo zilisema kuwa chama cha Kiliberali cha Waziri Mkuu huyo Koizumi kilishindwa kurejesha ule ushindi wake mkubwa wa kukiwezesha kutawala peke yake. Upande wa pili chama kishirika cha Kisoshalisti cha Kiliberali katika serikali hiyo ya mwungano kimenyakua hadi viti 205. Uchaguzi huo uliofanyika mapema ulikuwa kama mtihani kwa siasa ya marekibisho ya Waziri Mkuu Koizumi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW