1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali: Waliofariki ajali ya boti Kongo ni 34

10 Oktoba 2024

Ajali ya boti iliyotokea kwenye Ziwa Kivu tarehe 3 Oktoba imewauwa watu 34, kulingana na hesabu rasmi ya serikali iliyotolewa Alhamisi.

DR Kongo
Maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu wakibeba mwili ulioopolewaPicha: Ruth Alonga

Miili ya watu 11 kati ya 34 waliothibitishwa kufariki ilizikwa kwenye shamba la makaburi la makao, wilayani Nyiragongo, umbali kidogo kutoka mji wa Goma.

Hata hivyo, gesi inayoendelea kuwa kwenye Ziwa Kivu imekuwa kikwazo katika juhudi za kuopoa miili mingine inayozaniwa kuwa imekwama kwenye mabaki ya boti iliyojaa.

Mazishi ya watu 11 yalifanyika Jumatano

Mazishi ya watu hao 11 yalifanyika kwa huzuni kubwa mbele ya familia za waathirika katika mji wa Goma. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na jamaa na marafiki, ambao walionyesha majonzi yao na wasiwasi juu ya hatari inayowakumba kila siku. Hata hivyo, asasi za kiraia katika mikoa ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini zimeikosoa serikali kwa kushindwa kutoa hesabu kamili ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo.

Kahindo Bazungu, akiwa na huzuni kubwa, alilia akiyaangalia majeneza ya ndugu zake wawili, ambao walikuwa wakifadhiwa maiti kwa muda wa wiki moja.

Jamaa za walioangamia katika ajali ya boti Ziwa Kivu wakiliaPicha: Ruth Alonga

Mazishi ya watu hao 11, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Jumatano, yalifanyika huku mamia ya familia za waathirika zikihangaika kutafuta miili ya ndugu zao, ambao wanazaniwa kuwa wamekwama katika mabaki ya boti hiyo.

Juhudi zakuitafuta boti hiyo iliyo zama octaba 3 wiki iliyopita zinakumbana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya ukungu mzito, unaokwamisha kazia ya watafutaji.

Rushwa katika bandari za Ziwa Kivu

Kulingana na vyanzo vya ndani, boti hiyo ilikuwa imebeba mizigo na watu zaidi ya 400, jambo ambalo bado halijathibitishwa na mamlaka hapa nchini.

Katika hotuba yake mbele ya umati wa watu, Jean Jacques Purusi, gavana wa Kivu Kusini, alikemea vikali ongezeko la rushwa miongoni mwa idara mbalimbali za serikali kwenye mabandari ya Ziwa Kivu, akisema kuwa hii ni moja ya sababu zilizoleta ajali hiyo.

Matukio haya yanajiri wakati ambapo waziri wa uchukuzi wa DRC, Jean Pierre Bemba, ametangaza kusimamisha safari za usiku kwenye Ziwa Kivu. Tangazo hili limewashitua baadhi ya wasafiri wanaotumia Ziwa Kivu kwa safari za usiku, huku wengi wakitazamia mabadiliko haya katika usafiri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW