1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Bashar Al Assad yadaiwa kuondolewa madarakani

8 Desemba 2024

Serikali ya Bashar Al Assad huenda ikawa imeondolewa madarakani baada ya waasi kutangaza kuudhibiti mji wa Damascus, huku shirika la upinzani la uangalizi wa vita likiripoti kwamba Rais Assad ameikimbia nchi hiyo.

Syria
Serikali ya Bashar Al Assad yadaiwa kuondolewa madarakaniPicha: Orhan Qereman/REUTERS

Kulingana na mkuu wa shirika hilo, linaloangazia pia masuala ya haki za binaadamu, Rami Abdurrahman, rais Assad aliabiri ndege hii leo (08.12.2024) asubuhi kutoka Damascus na kuondoka nchini.

Hata hivyo hadi sasa serikali ya Syria, haijatoa taarifa yoyote rasmi juu ya kuondoka kwake. 

UAE yaitolea mwito Syria kujizuwia na vurugu

Hii ni mara ya kwanza wapiganaji wa upinzani kuingia Damascus tangu mwaka 2018 wakati vikosi vya Syria vilipoyatwaa tena maeneo yalio nje ya mji huo kufuatia mzingiro wa mwaka mmoja.

siku moja kabla ya kuingia Damascus, waasi hao waliudhibiti mji wa Homs, mji wa tatu kwa ukubwa nchini humo huku vikosi vya serikali vikiuhama mji huo. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW