DRC: Serikali yaondoa uwezekano wa kurudiwa kwa uchaguzi
28 Desemba 2023Matangazo
Matokeo ya uchaguzi huo wa Desemba 20 yanaonyesha kuwa Rais aliyeko madarakani Felix Tshisekedi anaongoza kwa tofauti kubwa dhidi ya wapinzani wake.
Hali ya mvutano unaozidi kuhusiana na uchaguzi huo inatishia kuivuruga zaidi Kongo, ambayo tayari inapambana na mzozo wa usalama katika maeneo ya mashariki.
Hapo jana polisi mjini Kinshasa ilivunja maandamano ya watu wanaopinga namna uchaguzi wa rais na bunge ulivyoendeshwa.
Upinzani unasema uchaguzi huo ulikumbwa na kasoro nyingi na udanganyifu, madai ambayo tume ya uchaguzi, CENI inayakanusha.
Muyaya amesema wapinzani wanapaswa kusubiri hadi matokeo kamili yatangazwe ndiyo wayapinge katika mahakama ikiwa hilo litahitajika.