Serikali ya Ethiopia yatishia kufanya operesheni tena Tigray
15 Julai 2021Matangazo
Hali hiyo inatishia hatua iliyotangazwa na serikali ya kusitisha mapigano katika eneo hilo linalokabiliwa na mgogoro.
Vikosi vya waasi wa Tigray wiki hii vilidai kupata mafanikio zaidi baada ya kudhibiti sehemu kubwa ya mkoa huo wa kaskazini wiki mbili zilizopita ambapo vikosi vya Tigray viliudhibiti tena mji mkuu wa Tigray, Mekele baada ya eneo hilo kutumbukia kwenye vita kwa muda wa miezi minane.
Waziri Mkuu Abiy Ahmed, amesema serikali yake ilitangaza kusitisha mapigano mnamo Juni 28 kwa sababu ilichagua amani kwa matumaini kwamba mapigano yatasimama kabisa hali itakayowawezesha wakulima kupanda mazao ya chakula na wakati huo huo kuwezesha misaada kupelekwa katika mkoa huo uliokumbwa na vurugu.