Guinea yavifuta vyama 40 vya siasa
7 Machi 2026
Matangazo
Kulingana na agizo hilo vyama vilivyopigwa marufuku havitambuliki tena kisheria na vinapaswa kusimamisha shughuli zote mara moja. Vyama hivyo vimepigwa marufuku kutumia nembo zao, majina au alama, na mali zao zitataifishwa na kudhibitiwa na serikali.
Karibu miezi miwili baada ya Doumbuya kuingia mamlakani
Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni chini ya miezi miwili tangu kiongozi wa kijeshi Mamady Doumbouya alipoapishwa kuwa rais wa Guinea. Asasi za kiraia zimeukosoa uamuzi huo ziliouita wa kidikteta.
Vyama vilivyofutwa ni pamoja na UFDG kilichokuwa chini ya uongozi wa Cellou Dalein Diallo aliye uhamishoni, RPG cha Rais wa zamani Alpha Conde, na chama cha UFR.