Kenya kupinga uamuzi wa mahakama kuzuia polisi kwenda Haiti
26 Januari 2024Matangazo
Msemaji wa serikali, Isaac Mwaura, ameeleza katika taarifa yake kuwa serikali inaheshimu utawala wa kisheria na hivyo wamepanga kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.
Mapema leo, Mahakama Kuu ilitoa uamuzi wa kuizuia serikali kupeleka maafisa wa polisi nje ya nchi na kuitaja hatua hiyo kuwa kinyume na katiba.
Soma zaidi: Mahakama Kenya yaizuwia serikali kupeleka askari Haiti
Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita, amesema katika uamuzi wake leo kuwa jeshi la ulinzi la Kenya (KDF) ndilo pekee lenye uwezo wa kuongoza ujumbe wa amani nje ya nchi.