Serikali ya Kenya kupinga uamuzi wa mahakama kuhusu Haiti
27 Januari 2024Jaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya Enock Chacha Mwita, ameamua kwamba "uamuzi wowote wa chombo chochote cha serikali ama afisa wa serikali wa kupeleka kikosi cha polisi nchini Haiti unakiuka katiba na sheria hivyo basi ni kinyume cha sheria.''
Soma pia:Mahakama Kenya yaizuwia serikali kupeleka askari Haiti
Saa chache baadaye, msemaji wa serikali Isaac Mwaura alijibu kwa kusema kuwa wakati serikali inaheshimu utawala wa sheria, imefanya uamuzi wa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo mara moja.
Soma pia:Bunge la Kenya yaidhinisha polisi kutumwa nchini Haiti
Mwaura ameongeza kuwa serikali inasisitiza kujitolea kwake katika kuheshimu majukumu yake ya kimataifa.
Huku hayo yakijiri, Ekuru Aukot, mwanasiasa wa upinzani aliyepinga hatua ya kupelekwa kwa kikosi hicho cha polisi nchini Haiti, amesema yuko tayari kwa mapambano ya muda mrefu.