1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Sasa ruhusa kuzalisha mazao ya mbegu za GMO

Zainab Aziz Mhariri: Josephat Charo
4 Oktoba 2022

Baraza la mawaziri la Kenya limeubatilisha uamuzi wa kupiga marufuku uzalishaji wa mazao yaliyobadilishwa vinasaba baada ya marufuku hiyo kuwepo kwa muda wa muongo mzima.

Kenia wartet mit Spannung auf das Urteil des Obersten Gerichtshofs zu den Wahlen | William Ruto
Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Rais wa Kenya William, Ruto amesema Kenya sasa inaweza kuzalisha na kuagiza mahindi yaliyobadilishwa vinasaba baada ya miaka mingi ya wasiwasi nchini humo na barani Afrika kwa jumla juu ya usalama wa vyakula vya GMO yaani vyakula vilivyobadilishwa asili yake.

Bunge la KenyaPicha: Simon Maina/AFP via Getty Images

Baraza la mawaziri  la Kenya lilijadili baa la ukame ambalo limeziathiri kaunti 23 kati ya 47 za Kenya. Mawaziri hao pia walijadili mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa manufaa ya watu zaidi ya milioni 50 wa nchi hiyo. Walijadili njia za ufanisi juu ya kuleta mageuzi katika mfumo wa kilimo nchini Kenya kwa kuweka mkazo juu ya kuzalisha mazao yenye uwezo wa kustahimili magonjwa. Bi Maimuna Mwidau ni mchambuzi wa mswala ya kijamii na kisiasa nchini Kenya na mwanaharakati wa kundi linalotetea kilimo cha mbegu asilia ana haya ya amesema ni vyema serikali ya Kenya itilitile maanani mbinu za kuwezesha kilimo cha umwagiliaji badala ya kufanya maamuzi yanayoweza kuleta athari zaidi kwa Wakenya na mazingira ya nchi hiyo.

Wanyama wanakufa kutokana na ukame uliokithiri katika baadhi ya maeneo ya mpakani kati ya Kenya na Ethiopia.Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Kilimo ndiyo msingi muhimu wa uchumi wa Kenya ambapo aslimia 70 ya watu kwenye sehemu za mashambani wanashughulika na kilimo. Rais wa Kenya William Ruto anakusudia kuongeza tija kubwa katika sekta ya kilimo. Nchi nyingi za Afrika zimepiga marufuku kilimo cha mazao yaliyobadilishwa vinasaba kutokana na hofu ya kuwaathiri wakulima wadogo wadogo, kuathiri mazingira na afya za watu.

Waandamanji wanaopinga uzalishaji wa mazao yaliyobadilishwa vinasaba nchini Marekani.Picha: DW

Mapema mnamo mwaka huu Marekani kupitia kwa wawakilishi wake wa biashara, iliikosoa Kenya juu ya uamuzi wake wa kupiga marufuku mazao ya kilimo ya Marekani kuingia Afrika Mashariki. Ofisi ya biashara ya Marekani imesema katika ripoti yake ya mwaka kwamba hatua hiyo ya marufuku imeathiri msaada wa chakula. Ujumbe wa Marekani uliohuduria kuapishwa kwa rais William Ruto ulitilia maanani msimamo wa rais Ruto juu ya kuunga mkono vipaumbele vya Afrika ikiwa pamoja na kuimarisha biashara ya pande mbili.

Chanzo:AP