Serikali ya Kongo na M23 zasaini makubaliano ya amani
15 Novemba 2025
Matangazo
Kuanzia mwezi Aprili mwaka huu, Qatar iliandaa na kusimamia raundi kadhaa za mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali ya Kongo na waasi hao wa M23 na tangu wakati huo kumekuwa kukijadiliwa masharti ya awali pamoja na kujenga mazingira ya pande hizo hasimu kuaminiana.
Pande hizo mbili zilisaini mwezi Julai tamko la kanuni ambalo halikuweka wazi namna ya kushughulikia masuala mengi muhimu ambayo ndiyo chanzo cha mzozo huo, na mwezi Oktoba hatimaye mahasimu hao walifikia makubaliano kuhusu hatua za ufuatiliaji wa kusitisha mapigano.