MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Waasi wa ADF washutumiwa kwa kushambulia migodi na kuua raia
16 Machi 2026
Matangazo
Taarifa hii ya jana Jumapili ya serikali imesema ADF linalodai kuwa na mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, Jumatano iliyopita lilivamia migodi ya dhahabu iliyo karibu na mikoa ya Muchacha na Ituri.
Kulingana na serikali, shambulizi hilo ambalo IS ilidai kulifanya lilisababisha vifo vya raia baadhi ya majengo kuungua na wakazi wengi kuyakimbia makazi yao.
Kundi la ADF lililoanzishwa na waasi wa nchini Uganda limekuwa likishutumiwa kwa mauaji ya halaiki na uporaji huko Ituri na jimbo jirani la Kivu Kaskazini, katikati ya machafuko yaliyogubika mashariki mwa Kongo.