Serikali ya Mali yafunga kituo cha televisheni cha kibinafsi
23 Novemba 2024Matangazo
Afisa mmoja wa kituo hicho aliyezungumza kwa msaharti ya kutotajwa jina lake aliliambia shrika la habari la AFP kwamba mamlaka ya mawasiliano ya Mali ilizuia leseni ya Joliba TV News kuanzia tarehe 26 Novemba. Hatua hiyo inafuatia malalamiko yaliyowasilishwa dhidi ya kituo hicho Novemba 12 na mamlaka ya mawasiliano ya Burkina Faso kuhusu maoni yaliyotolewa na mwanasiasa wa Mali Issa Kaou N'Djim kuhusu serikali ya Burkina Faso yenyewe. Anatarajiwa kushtakiwa kwa kumkashifu hadharani mkuu wa nchi ya kigeni Desemba 23. Mataifa hayo mawili ya Afrika Magharibi yanatawaliwa na tawala za kijeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2020 na 2022, yakiungana na Niger inayoongozwa pia kijeshi ambayo yameunda shirikisho la Muungano wa Nchi za Sahel (AES).