1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Serikali ya Netanyahu kuapishwa

29 Desemba 2022

Serikali mpya ya Benjamin Netanyahu inatarajiwa kuapishwa leo mjini Jerusalem ikiwa ni baada ya miezi miwili baada ya waziri mkuu huyo mteule kushinda uchaguzi wa bunge nchini Israel.

Benjamin Netanjahu
Picha: Abir Sultan/Pool EPA/AP/dpa/picture alliance

Hii ni serikali ya siasa za mrengo wa kulia zaidi ambayo Israeli imewahi kuwa nayo, huku wanasiasa wa siasa kali za mrengo huo pia wakijumuishwa kwa mara ya kwanza katika serikali ya mseto. Serikali hiyo mpya inataka kutekeleza mabadiliko mapana ya kisiasa na, pamoja na mambo mengine, kuudhoofisha kwa makusudi mfumo wa mahakama nchini Israel. Kulingana na wataalamu, mabadiliko hayo yanaweza pia kusababisha kufutwa kesi ya ufisadi inayoendelea kwa sasa dhidi ya Waziri Mkuu Netanyahu. Hii ni serikali ya sita iliyoundwa na kiongozi wa kihafidhina wa chama cha Likud, Benjamin Netanyahu. Waziri mkuu huyo wa zamani anarejea madarakani baada ya mwaka mmoja na nusu kwenye upinzani.